Iringa yafanya ukaguzi wa magari na madereva barabarani

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Mrakibu wa Polisi Glory Mtui amewakumbusha wamiliki wa vyombo vya moto kufuatilia mienendo ya vyombo vyao kwa kufanya marekebisho ya mara kwa mara ili kuepusha ajali zitokanazo na uchakavu wa magari hayo.

SP Mtui ametoa wito huo Septemba 22 mwaka huu  majira ya usiku alipofanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye barabara kuu ya Iringa - Mbeya ili kubaini changamoto mbalimbali hasa nyakati za usiku.

Ukaguzi huo ambao ulifanikisha kukagua zaidi ya mabasi 40 ya abiria na malori ya mizigo zaidi ya 50 ulihusisha uhakiki wa hali ya magari, nyaraka muhimu za usafiri, na upimajï wa kiwango cha kilevi kwa madereva ili kubaini kama wanaendesha wakiwa wamelewa ambapo zoezi hilo lililenga kuongeza usalama barabarani na kupunguza ajali kwa kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa kikamilifu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii