Hatima ya kesi ya rufaa waliyoikata Nyundo na wenzake watatu ya kupinga kifungo cha maisha gerezani itajulikana leo Septemba 25 mwaka huu katika hukumu inayotarajiwa kutolewa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Wanaopinga hukumu hiyo ni pamoja na Clinton Damas, maarufu Nyundo, ambaye alikuwa ni askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) MT. 140105. Wengine ni askari Magereza C. 1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson (Machuche) na Amin Lema (Kindamba).
Nyundo na wenzake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kuwakuta na hatia kwenye mashtaka yaliyokuwa yanawakabili ya kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile Binti Mkazi wa Yombo Dovya Dar es salaam mwaka jana 2024.
Wakata warufani hao wanawakilishwa na mawakili watatu wa kujitegemea ambao ni Godfrey Wasonga, Roberth Owino na Meshack Ngamando huku upande wa Serikali ukiwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Lucy Uisso na wenzake wawili.