Bilioni 200 kutolewa kwa wafanyabiashara wadogo

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Samia Hassan Suluhu ameahidi Bilioni mia mbili (200) kwa wafanyabiashara wadogo wadogo Nchi nzima kwenye siku mia (100) za kwanza pindi  atakapoingia tena madarakani baada ya uchaguzi utakaofanyika Octoba 29 mwaka huu. 

Kwa mujibu wa ILO na mashirika washirika kama AU, UNDP na Briter Bridges,wa  kuendeleza wafanyabiashara wadogowadogo kusini mwa Jangwa la Sahara zinalenga kuzalishasha ajira kwa vijana, ambapo asilimia 71.7 ya vijana wenye umri wa miaka kati ya 25-29 wanafanya kazi zisizo rasmi.

ILO inapendekeza serikali zitenge kati ya dola 10,000 hadi 100,000 kama ruzuku (sawa na shilingi milioni 25-250) sambamba na kuanzisha vituo vya ubunifu na miundombinu ya kidigitali.

 Mpango wa Tanzania wa kutenga shilingi bilioni 200 unalingana na viwango vya chini vya mitaji ya awali vinavyotambuliwa na ILO, na kuiweka nchi katika nafasi ya juu kikanda kwa uwekezaji wa moja kwa moja kwa sekta ya ujasiriamali, fedha hii inaweza kuanzisha biashara mpya 400,000 kwa mtaji wa awali wa shilingi 500,000.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii