Msanii wa Kike katika soko la Rap, Cardi B amefunguka kuwa wasanii wengi wa kike
aliowasaidia walimgeuka, wakamsaliti mpaka kufikika hatua ya “Kuchepuka” na
Mume wake.
Akipiga
stori na msanii mwenzake Kelly Rowland, Cardi B lisema kuwa ni wasanii
wengi sana wa kike ambao amewasaidia katika soko la muziki na kupata mafanikio
makubwa, lakini mwisho wa siku alichoambulia ni kusalitiwa mpaka kufikia hatua
ya kumsaliti na mume wake (Japo hajataja ni nani).
Katika
maelezo yake, Cardi ameongeza kuwa, ilifikia hatua alikuwa akiwafuata wasanii
hao katika DM zao ili kuwahamasisha wapambane na kuwatia moyo Zaidi, ila mwisho
wake aliambulia maumivu ya moyo.
“Nilichokuja kugundua
na kujifunza, ni kuwa unakuwa mwema kwa mtu wa aina gani” alisema Cardi B
Rappa huyo
wa kike ambaye pia ni mshindi wa tuzo za Grammy, ametangaza kuachia Album yake
mpya aliyoipa jina la “AM I THE DRAMA?”
na itaingia rasmi sokoni SEPTEMBA 19,
2025