Zanzibar yazizima: Samia kunadi Ilani ya CCM leo

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, leo kunadi sera na ilani katika viunga vya Unguja, visiwani Zanzibar, wananchi wampokea kwa kishindo.

Ziara ya Dk. Samia Zanzibar inatazamiwa kuongeza msisimko wa kisiasa, huku wananchi wakingojea kwa matumaini ahadi na dira ya maendeleo kwa miaka mitano ijayo.

Ni kisiwa chenye sifa za kipekee, maarufu kwa mandhari ya kuvutia, historia ndefu ya biashara ya karafuu na utalii unaoipa sura ya kimataifa. 

Hapa ndipo Stone Town. Ukijulikana kwa majengo ya kihistoria na mitaa yenye harufu ya viungo.

Uchumi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa unategemea utalii, uvuvi, kilimo cha mwani na karafuu, ambazo zimekuwa zao kuu la biashara tangu karne nyingi. Serikali imekuwa ikihimiza uwekezaji, ili kukuza ajira kwa vijana na kuongeza mapato.

Aidha, visiwa hivi vinajulikana kwa vyakula vyake vya aina mbalimbali, vinavyochanganya ladha za Kiarabu, Kiswahili na Kihindi. Wali wa nazi, biriani, urojo, samaki wa kupaka na mishikaki ni miongoni mwa vyakula maarufu vinavyovutia wageni na wakazi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii