Miili ya masista wanne waliofariki ajalini Mwanza yaagwa leo Bagamoyo

Miili ya masista wanne wa waliofariki ajalini Mwanza ikiingizwa katika Kanisa la Mwenyeheri Isdory Bakanja Boko, Jimbo Katoliki Bagamoyo kwa ajili ya misa ya kuwaombea kabla ya maziko.

Masista hao, Lilian Kapongo, Damaris Matheka, Stellamaris Muthini na Nerina De Simone walifariki dunia Septemba 15, mwaka huu pamoja na dereva wao, Boniphace Msonola aliyezikwa Jana Septemba 18 Nyegezi jijini Mwanza.

Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Kanisa Katoliki, viongozi wa Serikali, ndugu, jamaa na waamini wa madhehebu mbalimbali waliokusanyika kuaga miili ya watumishi hao waliopoteza maisha wakiwa katika shughuli za kitume.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii