Prof, Nombo ashiriki maadhimisho ya siku ya mwalimu dunia wilaya ya Bukombe

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo, anashiriki Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani katika yanayofanyika Oktoba 3 mwaka huu katika Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.

Aidha, amepata fursa ya kuona shughuli Mbalimbali zinazohusu ustawi wa Walimu katika baadhi ya mabanda ya maony4sho yaliyopo katika viwanja hivyo.

Maadhimisho haya yanatoa fursa ya kutambua mchango mkubwa wa walimu katika maendeleo ya elimu na ustawi wa jamii, sambamba na kuhamasisha uwekezaji katika mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii