Wananchi wa Karatu, mkoani Arusha, katika shamrashamra za kumsubiria mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ambaye leo Oktoba 3 mwaka huu anatazamia kumalizia kampeni mkoani humo kisha kuelekea Katesh, wilayani Hanang', mkoani Manyara, kuendelea kunadi sera na ilani ya uchaguzi.
Akiwa katika mkoa huo amefanya mikutano mitatu huku akinadi sera na ilani ya uchaguzi na kuahadi kuwa pindi atakapo pewa nafasi nyingine atafungua jiji hilo katika katika kukuza utalii na kuongeza ajira zaidi kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na uchumi wa nchi.
Hata hivyo Agosti 28 mwaka huu Dk. Samia alizindua kampeni za chama hicho mkoani Dar es Salaam, kisha akaanza kuchanja mbuga kwenda mkoa kwa mkoa akianzia Mkoa wa Morogoro.
Kila mkoa Dk. Samia alitumia fursa za kiuchumi zinazopatikana kwa kueleza namna atakavyozitumia kuleta mabadiliko ya uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi wake.