MAADHIMISHO YA SIKU YA MWALIMU DUNIANI – USHIROMBO, GEITA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, amesema kuwa walimu ndio chachu ya ugunduzi, ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia kwa kizazi kipya, hivyo kazi ya kuwaendeleza walimu ni endelevu na ya kipaumbele.

Akihutubia mamia ya walimu na wananchi waliofurika kwa wingi katika viwanja vya shule ya Msingi Ushirombo, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Waziri Mkuu amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha walimu wanapata nyenzo za kisasa ili waweze kutoa elimu bora na yenye matokeo chanya zaidi.

Aidha, amesisitiza kuwa serikali inaendelea kutoa ajira kwa walimu, pamoja na kuwapandisha madaraja walimu waliopo kazini, ili kuhakikisha uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi unakidhi viwango vya sasa vya kimataifa.

"Rais Samia anataka kila mtoto wa Kitanzania apate elimu bora. Hili linawezekana kwa kuhakikisha mwalimu anathaminiwa, anapewa stahiki na mazingira bora ya kufundishia," amesema Mhe. Majaliwa.

Ikumbukwe kuwa "Siku ya Walimu Duniani si tukio la kawaida  bali ni siku yenye thamani kubwa kwetu sote.

Ingawa Walimu ndio msingi wa maarifa, maadili na maendeleo ya jamii. Tukumbuke kuwashukuru, kuwaheshimu na kuwaunga mkono daima katika bidii zao mashuleni.

Hata hivyo unapaswa kutambua kuwa Wewe uliyepo hapa hata uwe mwalimu nyuma yako kuna mkono wa mwalimu, chukuwa simu yako mtumie meseji mwalimu huyo mtakie "Heri ya Siku ya Mwalimu Duniani!" nakwambia kuna baraka unakwenda kuzipokea leo, kwani Mungu wetu naye anakuona" anasema Naibu Waziri Mkuu, Mbunge wa Bukombe Dkt Dotto Biteko.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii