Tuhuma za Utekwaji wa Humphrey Polepole Polisi Waanza Uchunguzi

Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa na Augustino Polepole kuhusu madai ya kutekwa kwa ndugu yake, Humphrey Polepole.

 Katika hatua hiyo Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi huo  unalenga kubaini kama kweli Humphrey Polepole alikuwa mkazi au mpangaji wa nyumba ambako inadaiwa tukio hilo lilifanyika.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi leo Oktoba 7 mwaka huu jalada la uchunguzi lilifunguliwa mara baada ya taarifa hizo kusambaa  Oktoba 6 mwaka huu.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mbali na kukusanya maelezo kutoka kwa watu mbalimbali, Polisi wanaendelea kumtafuta Augustino Polepole ili atoe ushirikiano na maelezo ya kina kuhusu madai hayo, ikiwemo uthibitisho wa madai yake kwamba Afisa wa Polisi alihusika katika tukio hilo.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, jijini Dodoma.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii