VISIT ILEMELA SEASON TWO YATOA MANUFAA KWA WANAKAYENZE.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amir Mkalipa amewataka Wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mnamo Oktoba 29 mwaka huu kulingana na vyama vyao.

Mkalipa ameyasema hayo katika Tamasha la Visit Ilemela season two lililofanyika Septemba 26 mwaka huu katika viwanja vya shule ya msingi Kayenze, Kata ya Kayenze Wilaya ya Ilemela, Tamasha lilioandaliwa na Wilaya hiyo likiwataka Wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu na kuitangaza Wilaya.

Amewataka Wananchi kujitokeza kupata huduma na Elimu mbalimbali zinazotolewa kutoka kwenye Mabanda ya wizara mbalimbali Ikiwemo Uvuvi, Maendeleo ya Jamii, Dawati la Jinsia, Kilimo, Afya, Time huru ya Taifa ya Uchaguzi na Mahakama.

Katika hatua nyingine Mkalipa amesema itawachukulia hatua Kali Wanafunzi watoro kutokana na Wilaya hiyo kuendelea kufanya vizuri katika sekta ya Elimu huku akiwataka Wazazi kutekeleza Uchangiaji wa Chakula Cha watoto shuleni kama walivyokubaliana kwenye vikao vyao.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ilemela, Ummy Mohammed Wayayu amesema wataendelea kutembelea kata zote 19 zilizopo nje ya Mji ili kusogeza huduma mbalimbali kwa Wananchi Bure.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Iseni kata ya Kayenze na Wananchi wameipongeza Wilaya hiyo kwa kuwasogezea huduma hizo karibu nao na kutaka Utaratibu huo uendelee kutokana na wengi wao kupata nyingi Bure na kwa haraka zaidi.

Tamasha la Visit Ilemela season 2 litaendelea tena Septemba 28 mwaka huu katika eneo la Igombe ndani ya Wilaya hiyo huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Amir Mkalipa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii