Kanisa Michigan lashambuliwa wanne wapoteza maisha

Kufuatia shambulio lililofanywa na  mtu mwenye silaha kari baada ya  kushambulia ibada katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Grand Blanc Township, Michigan, Jumapili asubuhi,Watu wanne wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa polisi wanasema. Mshukiwa aliuawa na maafisa waliojibu tukio.

Mamlaka zimetambua mshukiwa kuwa Thomas Jacob Sanford, 40, ambaye alidaiwa kulipiga gari lake kwenye milango ya kanisa kabla ya kutoka na kufyatua risasi kwa mamia ya waumini waliokuwa ndani kwa kutumia kile polisi walichokiita bunduki ya kivita.

Mkuu wa Polisi wa Grand Blanc Township, William Renye, amesema kuwa uchunguzi unaonyesha mshukiwa aliwasha moto kwenye kanisa kwa makusudi, na picha na video mtandaoni zinaonyesha kanisa likichomwa na moto.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii