Othman Masoud aanza ziara ya siku saba Pemba

Mgombea urais wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, ameondoka leo Unguja kuelekea kisiwani Pemba kwa ajili ya ziara ya siku saba yenye lengo la kujenga ushawishi na kupata ridhaa ya wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

Katika ratiba ya ziara hiyo, Othman anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya Pemba, ambapo atazungumza na wananchi kuhusu changamoto zinazowakabili na kuwasilisha dira ya ACT Wazalendo kwa Zanzibar mpya. Aidha, ataendesha mazungumzo na viongozi wa dini, viongozi wa kijamii pamoja na watu mashuhuri, ili kuwashirikisha moja kwa moja katika mchakato wa mabadiliko.

Akizingatia mchango wa kilimo, hususan kilimo cha viungo, Othman atakutana na wakulima wa spice kujadiliana nao njia za kuongeza thamani ya mazao na kuyageuza kuwa chanzo kikuu cha uchumi wa Zanzibar. Vilevile, atakutana na wazee wa Pemba, akiwapa heshima na nafasi ya kutoa busara zao kwa mustakabali wa taifa.

Akizungumza kabla ya kuondoka Unguja, Othman amesema:

 “Ziara hii ni ya kuwasikiliza wananchi wa Pemba na kupata maoni yao moja kwa moja. Tunataka kujenga Zanzibar ya usawa, mshikamano na maendeleo ya kweli, ambapo kila Mzanzibari ataona matunda ya rasilimali zake. Huu ni wakati wa kuikomboa nchi yetu na kuirudisha mikononi mwa wananchi.”

Wachambuzi wa kisiasa wameeleza kuwa ziara hiyo ni hatua ya kimkakati inayoongeza mvuto wa Othman Masoud kwa wananchi wa Pemba na Zanzibar kwa ujumla, huku akionekana kama kiongozi anayeibua matumaini mapya kwa wananchi waliochoshwa na changamoto za muda

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii