Jeshi la polisi mkoani Tabora
linawashikilia watu wanne akiwemo mganga wa kienyeji aliyekuwa akinunua
damu kwa shilingi 600,00 ikiwemo viungo vya binadamu ambavyo ni sehemu
za siri za wanawake na wanaume kwa ajili ya shughuli za Uganga
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani hapa ofisini kwake jana Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao(ACP)alisema kwamba katika
Operesheni ya kukamata watu waliofanya mauaji januari 21 mwaka huu kwa
kuumua mwanafunzi wa darasa la nne aliyekuwa anasoma shule ya Msingi
Tutuo mwenye umri wa miaka 14 ilifanikiwa katika wilaya ya Sikonge
mkoani hapa.
Alisema kwamba baada ya tukio hilo ufuatiliaji
ulianza na kufanikiwa kuwakata watu watatau waliotiliwa mashaka katika
mahojiano dhidi yao walimtaja mganga anayeusika kununua viungo vya
Binadamu .
Alisema kwamba baada ya kukamwatwa kwa mganga huyo wa
kienyeji na kufanyiwa mahojiano alikiri kuwa napelekewa viungo vya
binadamu ambavyo ni sehemu za sri za mwanamke na sehemu za sri za
mwanaume .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao
alisendelea kusema kwamba mganga huyo aliemtaja kwa majina mtu mwengine
ambaye jina limehifadhiwa na sehemu anapopatikana ambapo baada ya
taarifa hiyo juhudi za kumtafuta zilifanyika hadi kupelekea kukamatwa
kwake ambapo alihojiwa na katika mahojiano ya awali amekiri kuhusika
katika utendaji wa matukio ya mauaji maeneo mbalimbali.
Alisema
kwamba baada ya kufanya mauaji uchukua damu kwa kuwachoma na kitu
chenye incha kali katika shingo na kuchukua damu inayoruka na kuikinga
katika chupa ndogo na kisha damu hiyo huuzwa kiasi cha Tsh 600,000/=.
Kamanda
huyo wa polisi aliongeze kusema kwamba mtu huyo uchukua baadhi ya
viungo vya miili yao ambavyo huwa wanapeleka kwa waganga wa kienyeji
ambao huwa ndio wanaowaagiza na kisha kuwalipa fedha kulingana na
makubaliano.
Hata hivyo katika mahojiano hayo mtuhumiwa huyo
amewataja watu wengine ambao anashirikiana nao katika utekelezaji wa
mauaji hayo.
Alisema kwamba mpaka sasa watuhumiwa wanne tayari
wamekamatwa na upelelezi unaendelea ili kufikia lengo la kuukamata
mtandao wote wa watu wanaohusika na mauaji ambapo majina yao
yamehifadhi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.