Zanzibar kuimarisha uchumi wa buluu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya sekta ya Uchumi wa Buluu ili wananchi wananufaika zaidi na kuongeza kipato chao.

Akizungumza na wavuvi wakulima wa mwani na wananchi katika Bandari ya Mkoani Rais Mwinyi alisema sekta ya uvuvi na kilimo cha mwani ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa sera ya Uchumi wa Buluu.

Rais alisema Serikali ya Awamu ya Nane inaendelea kuwajengea uwezo wakulima na wavuvi kupitia utoaji wa vifaa vya kisasa, ujenzi wa masoko na madiko, pamoja na mafunzo ya kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao yao. 

Aidha alisema Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo diko na soko la Mkoani pamoja na kiwanda cha mwani cha Chamanangwe kwa lengo ni kuwaandalia wakulima mazingira bora ya uzalishaji.

Rais Mwinyi alisisitiza kuwa Serikali itaendeleza ujenzi wa miundombinu ya Uchumi wa Buluu katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba, ikiwemo Bandari ya Shumba, soko la Kiwani na kiwanda cha kusarifu mwani cha Chokocho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii