Mahakama ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mohamed Hassan Nahero mwenye umri wa miaka 55, mkazi wa Kijiji cha Chingulungulu Kata ya Namatutwe Wilaya ya Masasi baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya bhangi Kg 6.4.
Mtiwahatiani alikamatwa Oktoba 28 mwaka huu akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya bhangi kwa kutumia baiskeli kutoka katika Kijiji cha Chingulungulu kuelekea Masasi mjini.
Katika utetezi wake mtiwahatiani amekiri kutenda kosa hilo kwa lengo la kujipatia kipato.
Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 08 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi Mhe Aisha Ndosy na Mwendesha mashtaka wa serikali Alex Samata