SIMBACHAWENE AVIOMBA VYOMBO VYA HABARI KUFANYA UTAFITI JUU YA RUSHWA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene ameviomba vyombo vilivyopo chini ya wizara hiyo kufanya utafiti na kuja na suluhisho la kuondoa na kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi ikiwemo tuhuma za rushwa na kubambikiziwa kesi huku akilitaka Jeshi la Polisi nchini kushirikisha makundi mbalimbali katika kutoa elimu ili kupambana na uhalifu…….

Ametoa kauli hiyo katika ziara ya kikazi mkoani Kagera baada ya kupokea Taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo iliyowasilishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Blasius Chatanda  kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi oktoba huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Fatma Mwassa akivipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kulinda amani kipindi cha uchaguzi mkuu.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii