Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamisha Msaidizi Mwandanizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya amewataka Maafisa na askari na Polisi wasaidi waliochaguliwa kulinda vituo vya kupigia kura mkoani Ruvuma kuhakikisha wanachukua hatua kali na za kisheria kwa mtu yeyote atakaebainika au kujaribu kufanya uhalifu au kuvuruga amani kwa Wananchi kabla ya kuleta taharuki katika jamii na Tanzania kwa ujumla ili zoezi hilo liweze kumalizika kwa Usalama na utulivu.
Hayo ameyasema Oktoba 28 mwaka huu mara baada ya kutembelea Polisi Wilaya za Namtumbo na Tunduru lengo likiwa kufanya ukaguzi na kuwasisitisa Maafisa Wakaguzi na Askari wote kutambua majukumu yao ya kimsingi katika kuimarisha ulinzi katika maeneo yao ya kazi waliyopangiwa.
Sanjari na hilo pia amesisitiza na kuwataka Maafisa wakaguzi askari na Polisi wasaidizi watakaokuwa katika vituo vya kupiga kura kuhakikisha wanasimamia kikamilifu zoezi hilo sambamba na kuvilinda vituo vya kupigia kura kuwalinda Wananchi na wawakilishi wa vyama watakaokuwa vituoni kwa kujiamini na kutumia weledi wa hali ya juu huku wakihakikisha hali za Usalama katika vituo vyote inaimalika ipasavyo ili Wananchi waweze kushiriki zaoezi la upigaji kula kwa amani na Utulivu.