Wacomoro wote wenye shida za Saratani kuletwa nchini Tanzania

Rais wa Bunge la Comoro ambaye pia ndiye kiongozi wa pili katika Uongozi wa Dola nchini humo Mhe. Moustadroine Abdou mapema leo amesema kuwa atahakikisha wacomoro wote wenye shida za Saratani wanaletwa nchini Tanzania na kufikishwa katika Taasisi ya Saratani ocean road na kupata tiba stahiki.

Akizungumza katika ziara fupi aliyoifanya mapema leo katika Taasisi hiyo Mhe Abdou amesema amestaajabishwa na mashine za kisasa zilizopo hapo na kusema kuanzia sasa hakuna haja ya wacomoro kupoteza pesa za walipa kodi wao kupeleka wagonjwa Ulaya huku akisisitiza kuwa Taasisi ya Saratani ocean road inatosha kuwa mkombozi wake.

Katika hatuaa nyingine Mhe. Abdou amesisitiza kuwa ili kupata wateja wengi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na hata nje ya nchi ya Afrika ni vyema watanzania wakadumisha Amani iliyopo na kujiepusha na kila aina ya vurugu ambazo zinaweza kuleta sintofahamu.

Aidha amempongeza Dkt. Samia kwa kuwezesha Taasisi hiyo kuwa na vifaa hivyo na kuahidi nchi yake itashirikiana na Tanzania ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika sekta ya afya.

Aidha Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Said Yakubu amesema nchi ya Tanzania siku zote ipo tayari kwa ushirikiano waowote na Comoro hivyo amemtoa hofu Mhe Abdou kuhusu jambo hilo huku akisema kuwa uhusiano huu utaimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani ocean road Dkt. Diwani Msemo amemshukuru Mhe Abdou kwa ziara hiyo na kusisitiza kuwa ujio huo pia umekuwa ni wa kukuza ushirikiano zaidi hivyo ORCI haItaacha fursa yoyote itakayotokana na wananchi wa Comoro.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii