Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wazazi kuhakikisha wanafunzi wanarudi shule kwani hali ya usalama imeimarika tayari na kote kuko shwari kabisa.
Amesema hayo leo Novemba 06 mwaka huu alipokua akizungumza na waandishi wa habari baada ya kubaini uwepo wa mahudhurio duni ya wanafunzi kwenye shule za msingi na sekondari.
Hata hivyo amesema kuwa hakuna shida yoyote ya usalama kwa sasa na tayari wananchi wamerudi kwenye hali ya kawaida hivyo wanafunzi wanapaswa kurudi shuleni kuendelea na masomo na kujiandaa na mitihani ya upimaji na taifa.