TEF yawaomba Watanzania kuimarisha amani

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limewaomba wananchi kusimama pamoja kama taifa, kuzungumza na kujisahihisha, ili vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu zisitokee tena.

Katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile ilieleza jukwaa linafuatilia kwa karibu na limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Watanzania, wakiwamo wanahabari na wengine waliojeruhiwa.

TEF alifafanua kuwa jukwaa linarejea utamaduni wa taifa wa kuwa na amani, utulivu na kuakisi yaliyotokea yakazaa maafa hayo. “Tunafahamu yapo maumivu makubwa kila upande, ila tunaomba sasa tusimame pamoja kama taifa, tuzungumze na kujisahihisha, ili kamwe haya yasitokee tena katika ardhi ya Tanzania,” ilieleza taarifa hiyo.

Hata hivyo ilieleza kuwa TEF inatoa mwito kwa mamlaka kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha haki inatendeka na kuitaka serikali kuanzisha mchakato wa maridhiano haraka ili kuponya majeraha kwa pande zote, kuomba kila upande mchakato huo utakapoanza uwe tayari kushiriki kama nchi kumaliza kadhia hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii