Mfanyabiashara Jenifer Jovin Bilikwija ‘Niffer’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam leo hii.
Kufuatia hatua hiyo Mama mzazi wa Mfanyabiashara Jenifer Jovin Bilikwija (Niffer), Mwanaisha Isack amerekodi video fupi ya kumuombea Mtoto wake msamaha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kusamehewa makosa anayotuhumiwa nayo kwani yeye ndio tegemezi na anategemewa na familia.
Mama mzazi wa Niffer amesema kuwa kama familia wamekubaliana kuomba radhi kutokana na makosa aliyoyatenda ili aweze kusamehewa.
Itakumbukwa kwamba Polisi walithibitisha kumkamata Niffer Octoba 27 mwaka huu akituhumiwa kwa makosa ya kuhamasisha Watu kufanya fujo siku ya kupiga kura na hadi sasa bado amekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi.