NEC yafanya uteuzi wa Wabunge Viti Maalumu 115 kati ya 116 wanaostahili

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanya uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalumu 115 kati ya 116 wanaostahili kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa taarifa ya NEC uteuzi huo umefanyika leo, Novemba 7 mwaka huu kufuatia masharti ya Ibara ya 66(1)(b) na 78(1) za Katiba, zikisomwa pamoja na kifungu cha 112 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024.

Tume imesema kuwa nafasi moja iliyosalia ya Mbunge wa Viti Maalumu itajazwa baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Fuoni, Tanzania Zanzibar, na Jimbo la Siha, Tanzania Bara.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii