Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imefanya kikao chake cha 51 Novemba 6 mwaka huu katika makao makuu ya taasisi hiyo mkoani Morogoro.
Kikao hicho kililenga kujadili na utekelezaji shughuli za TOSCI kwa kipindi cha Robo ya Kwanza (Julai - Septemba) ya Mwaka 2025/2026.
Aidha Bodi hiyo imejadili umuhimu wa kufanya mabadiliko ya sheria zinazosimamia ubora wa mbegu, pamoja na kutoa elimu kwa watumishi na wadau kuhusu miongozo mipya iliyoidhinishwa ili kuendana na mahitaji ya Taifa na wadau katika kuendeleza tasnia ya mbegu.
Aidha bodi imesisitiza na kuelekeza Menejimenti ya TOSCI iendelee kuhakikisha kuwa mbegu zote zinazozalishwa na sekta binafsi na umma zinatambulika rasmi na kuthibitishwa na TOSCI ili kudumisha ubora na uhalisia wa mbegu nchini kwa ajili kuwezesha kwakulima kuendelea kupata mbegu kwa kilimo biashara.