Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameielekeza Wizara ya Afya kusimamia na kutekeleza maelekezo ya kutozuia maiti katika Hospital na vituo vya afya nchini.
Aidha Dkt, Samia ametoa agizo hilo leo Novemba 14 wakati akilihutubia Bunge la 13 mwaka huu katika hafla ya kulifungua rasmi na kueleza mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha pili cha miaka mitano ijayo.
Hata hivyo ameziagiza Wizara ya Afya kusimamia maelekezo ya kutozuia maiti kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wakati familia zikiendelea na taratibu za kulipa deni kwa njia zinazolinda utu wao.