Wayahudi watakiwa kuhamia Israel kuepuka chuki

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Israel Gideon Saar amewatoa mwito kwa Wayahudi waishio kwenye mataifa ya magharibi kuhamia nchini Israel ili kuepuka chuki inayoongezeka dhidi ya jamii hiyo.

Akizungumza kwenye tukio la kuwasha mishumaa kukamilisha tamasha la Kiyahudi liitwalo Hanukkah Saar amesema kuwa ingawa Wayahudi wanayo haki ya kuishi kwa usalama kote kote duniani hivi sasa lakini jamii hiyo ikiwemo kwenye mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Australia, Canada na Ubelgiji "imekuwa ikiwindwa".

Saar ametoa matamshi hayo wiki moja baada ya Wayahudi 15 kupigwa risasi na kuuawa kwenye mkusanyiko wa kuadhimisha tukio la kidini mjini Sydney, Australia.

Hata hivyo tangu kuzuka vita vya Gaza vilivyofuatia shambulizi la kundi la Hamas la Oktoba 07, 2023, viongozi wa Israel wameonya mara kadhaa kuwa chuki dhidi ya Wayahudi inaongezeka kwenye nchi za magharibi na kuzituhumu serikali za mataifa hayo kushindwa kudhibiti hali hiyo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii