Bunge
limeendelea na vikao jijini Dodoma na mjadala ulikuwa kuhusu taarifa ya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Taarifa ya
kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu
Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021.
Miongoni mwa wabunge liochangia ni pamoja na mubunge wa Nzenga Vijijini Dk.Hamis Kingwangalla,alichangia hoja mbali mbali kuhusu ufafanuzi wa CAG.
"mnamo april 6 mwaka 2020 CAG aliwasilisha taarifa kuhusu ukaguzi wa fedha za serikali kuu kwa mwaka unaoishia june30 mwaka 2020 na katika uwasilishaji wake hapa bungeni CAG alinitaja kwa jina lakini vile vile alinitaja kwa nafasi niliyokuwa nashika hadi kufikia mwaka 2020 disemba nafasi ya waziri wa maliasili na utalii akiniusisha na hatua mbali mbali za kiupungufu ya kiutendaji yaliyoptokea katika wizara niliyokuwa naisimamia"