Shambulio la kijeshi la Urusi dhidi ya Ukraine "linaweza kuwa mwanzo wa mwisho" kwa Rais Vladimir Putin, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Lizz Truss amesema.
Lizz lisema "tunaona upinzani mkali na ushujaa wa Ukraine" na Uingereza "itaendelea kuwapa silaha na msaada wa kiuchumi".
Alisema anaamini kuwa Putin "anafanya makosa ya kimkakati" kutokana na uharibifu ambao vikwazo vya magharibi vitafanya kwa uchumi wa Urusi.
Lakini alipendekeza kwamba vita vinaweza kuendelea kwa "miaka kadhaa", na kuongeza: "Hii haitatokea - ninaogopa - haraka."
"Ninahofia mzozo huu unaweza kuwa wa umwagaji damu sana," alisema.
Alipoulizwa kuhusu vikwazo vya Uingereza, Truss alisema "amekusanya orodha ya watu wengine" na kupendekeza kutakuwa na "mpango wa vikwazo zaidi ".
Vita nchini Ukraine vitasababisha "gharama ya kiuchumi" kwa Uingereza, alisema. Lakini, alisema, watu wa Uingereza wataelewa bei ambayo tutalipa ikiwa hatutasimama dhidi ya Putin sasa.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza - tutamuunga mkono raia wa Uingereza wanaotaka kuelekea kupigana Ukraine
Hapo awali, tulimsikia Rais wa Ukrainia Zelensky akiwahimiza wapiganaji kutoka ng'ambo kujiunga na "jeshi la kigeni" lililoundwa hivi karibuni kuisaidia Ukraine katika vita .
Na asubuhi ya leo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Liz Truss, alisema ikiwa Waingereza watachagua kibinafsi kuelekea Ukraine kujiunga na vita, atawaunga mkono "kabisa ikiwa ndivyo wanataka kufanya".
Hapo awali Uingereza iliwashtaki watu waliosafiri kwenda Mashariki ya Kati kupigania au dhidi ya IS.
Shirikisho la Kimataifa la Judo limemsimamisha Vladimir Putin kama rais wa heshima na balozi.
Rais wa Urusi ana mkanda mweusi wa judo.
Uamuzi huo ni mojawapo ya "vikwazo" vya michezo vilivyotangazwa katika siku za hivi karibuni.
Mashindano ya Formula 1 Grand Prix ya Urusi, yaliyotarajiwa kufanyika mjini Sochi mwezi Septemba, yameghairiwa.
Na mapema ilitangazwa kuwa fainali ya Ligi ya Mabingwa ya 2022 itachezwa Paris badala ya St Petersburg.