Gachi Amshutumu Yammi Kwa Kuvunja Mahusiano Yake

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Fatma Omary ‘Gachi’ hivi karibuni ameibuka hadharani na madai mazito yanayomhusisha rafiki yake wa karibu, Yammi, katika kuvunjika kwa mahusiano yake ya kimapenzi.

Kupitia kauli yake iliyojaa hisia, Gachi amesema alimtambua Yammi kwa mpenzi wake kwa nia safi na kwa kuamini urafiki wao, bila kujua kuwa hatua hiyo ingegeuka chanzo cha maumivu kwake baadaye.

“Nilimtambulisha Yammi kwa mpenzi wangu lakini ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuvunjika kwa huba langu na mwanaume wangu. Bila shaka alitumia nguvu za asili maana sielewi hadi sasa jinsi alivyofanikisha mpango wake wa kuniibia mwanaume,” amesema Gachi.

Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa muziki, wengi wakitafakari juu ya mipaka ya urafiki, uaminifu, na changamoto za mahusiano ndani ya tasnia ya burudani.

Hadi sasa, Yammi hajatoa tamko rasmi kujibu tuhuma hizo, jambo linaloacha maswali mengi bila majibu.

Msanii wa Bongo Fleva, Yammi

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii