Bahati apima DNA na mwanamke anaedaiwa kuwa ni Mama yake

MWANAMUZIKI kutoka nchini Kenya Bahati hatimaye amekutana na mwanamke anayedaiwa kuwa ni Mama yake Judith Makokha na kuchukua hatua ya kwenda kupima naye vinasaba (DNA).

Mwisho wa mwaka 2025, mwanamuziki huyo alizungumzia suala hilo baada ya mwanamke huyo kusambaa kwenye mtandao ya kijamii akidai kuwa yeye ndiye Mama yake Bahati.

Judith alitoa video iliyosambaa akimuomba Bahati msamaha kwa madai ya kumtelekeza zamani. Aliongeza kuwa miaka mingi iliyopita hakuwa na uwezo wa kifedha wa kumtunza mwanawe, na kwamba alilazimika kumwacha katika kituo cha watoto yatima.

Bahati alivutiwa na simulizi ya Judith lakini alisisitiza kuwa aliwahi kushuhudia mazishi ya Mama yake mzazi miaka iliyopita.

Bahati alikuwa na mashaka kwa sababu alikulia akijua anatoka kabila la Wakamba ilhali mwanamke huyo ni Mluhya

Pia aligundua kuwa mwanamke huyo alikuwa akijaribu kuwasiliana na ndugu yake kwa miaka kadhaa, jambo lililomfanya amuonee huruma.

Wakenya walimlinganisha Judith na watoto wa Bahati, huku baadhi wakisema kuna mfanano. Jambo lililosababisha Bahati kuwasiliana na mwanamke huyo.

Hivi karibuni, alimuita na kuahidi kukutana naye, na kwamba walipokutana, alimnunulia bidhaa za matumizi ya nyumbani. 

Mama huyo alieleza jinsi alivyodaiwa kumwacha Bahati katika makao ya watoto zamani.

“Nilikutana na mwanamke fulani, na tuliishi nyumba moja. Huniumiza wakati mwingine nikifikiria kuhusu hilo; ndiyo maana sipendi kukumbuka. Wakati fulani mwanamke huyo aliniambia hataweza kunihudumia nikiwa na mtoto.

“Nilimwambia Mungu kuwa siwezi kurudi nyumbani. Nilipokuwa karibu kujifungua, niliondoka, na nilipofika Waruku, kulikuwa na wanawake walionionea huruma na kunisaidia. Nikaenda na mmoja wao nikiwa na mtoto wangu.

“Mmoja wa wanawake hao alinipa ushauri, akiniambia kuna mahali naweza kumweka mtoto wangu na nitakapokuwa sawa, nitamchukua,” alisimulia.

Alimtoa mtoto wake kwa matumaini kwamba angerudi kumchukua atakapokuwa amejisimamia kifedha.

Alieleza kuwa aliporudi kumchukua mtoto wake, aliambiwa kuwa mtoto huyo hakuwa tena hospitalini, jambo lililomvunja moyo. “Nataka tufanye DNA. Kila ninapokuona, nahisi tumboni mwangu kuwa wewe ni mtoto wangu,” alimwambia Bahati.

Bahati alikuwa amemnulia bidhaa za matumizi ya nyumbani baada ya kukutana naye kwa mara ya kwanza, na pia walifanya kipimo cha DNA.

“Kwa sasa sina matarajio maalum. Natarajia chochote, na kama ningekuwa na matarajio fulani, nisingekuja. Nilimsikiliza na hadithi yake ni ya kweli. Yeyote anayemjua Mama na Baba wa mtoto wake ni Mama.

“Ana imani kubwa, na sikutaka kuipuuzilia mbali kabla ya kufanya uchunguzi wangu wa kina na jambo la kisayansi. Tulitaka kituo kitakachotupatia matokeo ya kweli, na matokeo yanatarajiwa kutoka baada ya siku 14,” alisema Bahati.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii