Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi katika utekelezaji wa mapendekezo ya Tume za Rais kuhusu mgogoro wa ardhi na uhamaji wa hiari Ngorongoro kwa maslahi yao na nchi kwa ujumla.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo, leo Machi 12, 2026, wakati wa hotuba yake, katika hafla ya kupokea taarifa ya Tume za Rais kuhusu mgogoro wa ardhi na uhamaji wa hiari, Ngorongoro.
“Tumesikia kwamba Serikali tulifanya kwa nia njema lakini tulikosea baadhi ya maeneo na hayo ndio ya kukaa kutafakari na kuona namna ya kurekebisha,” amesema.
Amesema ni matumaini yake mapendekezo yaliyomo ndani ya taarifa hiyo, yataiongoza Serikali kupata namna bora ya kushughulikia jambo hilo kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu isimamie utekelezaji wa mapendekezo hayo na yaratibiwe kwa kushirikiana na Katibu Mkuu Kiongozi.
Amesema anatambua mchakato wa utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na tume unaweza kuibua mitazamo tofauti katika jamii hasa kutoka kwa wale wanaofaidika.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime