Mbunifu chipukizi mwenye kipaji kikubwa, Samia Khan, ameendelea kuvutia hisia za wengi baada ya kuonesha ubunifu wake wa kipekee katika jukwaa la Shindano la Top Model ndani ya Miss World Tanzania 2026.
Akiwa miongoni mwa wabunifu wachanga kabisa kushiriki, Samia ameonesha kuwa umri si kikwazo linapokuja suala la ubunifu na ndoto kubwa.
Katika onyesho hilo lililokusanya wadau wa mitindo, wanamitindo pamoja na mashabiki wa sanaa ya ubunifu, kazi za Samia zilijitokeza kwa upekee wake, zikichanganya mitindo ya kisasa na mguso wa utamaduni wa Kiafrika.
Mavazi yake yalipokelewa kwa shangwe kubwa, yakionesha ubunifu uliojaa ujasiri na maono mapya katika tasnia ya mitindo nchini.
Wengi walivutiwa na uwezo wake wa kubuni mavazi yanayoakisi haiba, nguvu na uzuri wa mwanamke wa Kitanzania, huku yakibaki na mvuto wa kimataifa. Ushiriki wake katika jukwaa hilo umefungua milango mipya na kuonesha wazi kuwa ana nafasi kubwa ya kuwa mmoja wa wabunifu wakubwa nchini na hata kimataifa.
Samia Khan sasa anatajwa kuwa miongoni mwa majina mapya yanayopaswa kufuatiliwa kwa karibu katika tasnia ya mitindo Tanzania.
Safari yake inaonekana ndiyo inaanza, lakini tayari ameacha alama isiyofutika kwenye jukwaa la Miss World Tanzania 2026.
katika Shindano la Top Model – Miss World Tanzania 2026