Pakistan imeendeleza leo maandalizi ya duru mpya ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran siku chache kabla ya makubaliano ya kusitisha mapigano kukamilika.
Rais wa Marekani Donald Trump
amesema wapatanishi wa Marekani wataelekea Pakistani leo, lakini haijabainika
wazi kama mipango hiyo itabadilika.
Kwa upande wake, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran
Esmail Baghaei, amewaambia waandishi wa habari mjini Tehran leo kwamba hakuna maamuzi
yaliofikiwa kuhusu mazungumzo hayo.
"Kwa sasa, nikiwa nahudumu, hatuna mipango ya awamu
inayofuata ya mazungumzo, na hakuna uamuzi wowote uliotolewa kuhusu hili."
Huku hayo yakijiri, China imeelezea leo wasiwasi kuhusu hatua ya Marekani ya kukamata meli yenye bendera ya Iran iliyojaribu kukwepa kizuizi cha majini, na kuzitaka pande zote mbili kurejelea mazungumzo ya amani.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime