Wapalestina waishio katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel, pamoja na wanaoishi kwenye eneo la katikati mwa Ukanda wa Gaza wanapiga kura Jumamosi 25.04.2026 katika uchaguzi wa manispaa ingawa uchaguzi huo ni wa kwanza tangu vita vilipozuka kwenye ukanda wa Gaza mwezi Oktoba, 2023.
Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Palestina yenye makao yake mjini Ramallah, takribani wapiga kura milioni 1.5 wamejiandikisha katika Ukingo wa Magharibi, na wengine takribani 70,000 wamejiandikisha kushiriki kupiga kura kwenye eneo la Deir el-Balah mjini Gaza.
Aidha uchaguzi wa huo unahusisha zaidi wagombea wanaoungwa mkono na chama cha Fatah cha Rais Mahmud Abbas, pamoja na wagombea huru.
Hata hivyo hakuna wagombea kutoka chama cha Hamas, ambacho kinadhibiti sehemu kubwa ya Ukanda wa Gazaa.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime