Baada ya mashambulizi ya Urusi dhidi ya Kyiv nchini Ukraine jana usiku, Ufaransa imeomba mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Waziri wa Ufaransa wa Ulaya na Mambo ya Nje, Jean-Noël Barrot, amelaani mashambulizi hayo kama "uhalifu" na kutaja vifo vya raia na uharibifu wa balozi mbili, zile za Austria na Uholanzi.
Mashambulizi ya usiku wa kuamkia Ijumaa, Novemba 20, 2026, yalisababisha vifo vya watu wasiopungua wanane nchini kote, wakiwemo sita mjini Kyiv.
Daraja mbili mjini Kyiv zimeharibiwa, na balozi za Austria na Uholanzi zimeguswa na mashambulizi hayo.
Barrot amesema kuwa "Urusi itapaswa kuwajibika" katika Baraza la Usalama na akaongeza kuwa Ufaransa haitalegeza shinikizo.
Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk, amelaani kile alichokiita "uchokozi" wa Urusi baada ya angalau kombora moja la Urusi kuanguka nchini Poland, ambayo ni mwanachama wa NATO na Umoja wa Ulaya. Alisema uchokozi huo "unaweza kuhusiana na mazoezi ya kijeshi yanayoendelea katika ardhi ya Poland" yanayohusisha nchi washirika wa Kyiv.
Waziri wa Ulinzi wa Poland, Władysław Kosiniak-Kamysz, ameeleza kuwa kombora la Kh-101 lilianguka mjini Nowy Lipowiec. "Katika tukio jingine, tunaweza pia kuzungumzia kombora, na katika tukio la tatu, uwezekano mkubwa wa ndege isiyo na rubani," aliongeza, akitaja maeneo matatu yaliyokumbwa na tukio hilo.
Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte, amelaani "ukiukaji mkubwa" wa anga ya Poland, nchi mwanachama wa Muungano huo Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte alilaani "ukiukwaji mkubwa" wa anga ya Poland.
Rais wa Urusi alionya kwamba nchi yake italipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya Ukraine, akiahidi kulipiza kisasi kikubwa zaidi. Tangu jana, mashambulizi ya mvamizi huyo yamekuwa makali. Matukio haya yanazidi kuonyesha kutokuwa na maana kwa "tamko la kuunga mkono amani" lililopitishwa siku ya Alhamisi na Xi Jinping, Vladimir Poutine, na Donald Trump.