Rais Samia Azungumzia Katiba Mpya, Maridhiano na Uchumi wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuunda Tume ya Maridhiano ya Kitaifa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kurejesha mshikamano, kuimarisha umoja wa Taifa na kuweka msingi wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Amesema Serikali imeanza mashauriano na makundi mbalimbali ya kijamii, yakiwemo viongozi wa dini, vyama vya siasa na taasisi za kiraia, kwa lengo la kupata wawakilishi watakaoshiriki katika Tume hiyo, ambayo inatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Amesisitiza kuwa Tume hiyo itakuwa na jukumu la kusaidia kulirudisha Taifa pamoja, kutambua hoja na changamoto zinazowakabili wananchi, pamoja na kujadili maeneo yanayohitaji mabadiliko katika Katiba.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii