Viongozi wakuu wa Iran wanadaiwa kuingia katika hali ya tahadhari kubwa ya kiusalama kufuatia hofu ya mashambulizi mapya baada ya vita vya hivi karibuni vilivyoihusisha Marekani na Israel.
Kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari nchini humo Kiongozi Mkuu wa Iran Mojtaba Khamenei anatajwa kuwa mafichoni katika eneo la siri lisilojulikana huku akitumia wajumbe maalum kufikisha maelekezo yake kwa viongozi wengine wa serikali.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa hatua hizo zimechukuliwa baada ya operesheni za kijeshi zilizodaiwa kuwaua baadhi ya viongozi waandamizi wa Iran, jambo lililosababisha mfumo mzima wa ulinzi na mawasiliano kubadilishwa kwa tahadhari kubwa.
Hata hivyo inaelezwa kuwa hata viongozi wa juu ndani ya Iran hawana mawasiliano ya moja kwa moja na kiongozi huyo huku taarifa nyingi zikisafirishwa kwa siri kupitia watu maalum ili kuficha eneo alipo.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime