Rais Hichilema aongoza kwenye matokeo ya kura

Rais Hakainde Hichilema anaongoza katika matokeo ya uchaguzi wa urais Zambia, baada ya zaidi ya nusu ya majimbo kutangaza matokeo yake.

Tume ya Uchaguzi imesema Hichilema amepata kura 1,544,140, sawa na asilimia 58.87, baada ya matokeo ya majimbo 135 kati ya 226 kuhesabiwa.

Mpinzani wake mkuu, Brian Mundubile amepata kura 1,030,662. Mgombea anahitaji zaidi ya asilimia 50 ya kura halali ili kushinda bila duru ya pili. Ingawa uchaguzi wa Alhamisi ulikuwa wa amani kwa kiasi kikubwa, upinzani umelalamikia vitisho, ukamataji na vurugu.

Zoezi la kuhesabu kura lilisitishwa kwa saa sita Ijumaa baada ya maafisa kushambuliwa na karatasi za kura kuibwa. Waangalizi wa kimataifa wamevitaka vyama kuepuka kauli za uchochezi kabla ya matokeo ya mwisho yanayotarajiwa kutangazwa leo Jumatatu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii