Ronaldo Aweka Wazi Mpango wa Kustaafu Soka

Staa wa timu ya Al Nassr, Cristiano Ronaldo 41 amesema kuwa huenda msimu wa 2026/27 huenda ukawa wa mwisho kwake kama mchezaji wa kulipwa baada ya kucheza kwa zaidi ya miaka 23.

Nahodha huyo wa Ureno  amesema anataka kuhitimisha safari yake akiwa ameacha urithi mkubwa katika mchezo wa  mpira  wa miguu.

 Katika mahojiano na jarida Vogue, Ronaldo alisema“Huu huenda ukawa mwaka wangu wa mwisho kucheza soka, na nataka kuacha urithi wa kipekee na wa kukumbukwa milele.”

Kauli hiyo inaashiria kuwa anaweza kutundika daluga baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa na Al-Nassr, unaofikia mwisho Juni 2027.

Ronaldo aliongoza Al-Nassr kutwaa ubingwa wa Saudi Arabia (Saudi Pro League) msimu uliopita akicheza mechi 30 akifunga magoli 28 na kutoa asisti 2.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii