Nchini Mali, idadi ya vifo vilivyotokana na shambulizi lililolenga kambi ya jeshi ya Dioura katika jimbo la Mopti, Alhamisi, imeongezeka.
Wanajeshi zaidi ya 10 wa jeshi la Mali, waliuawa, huku zaidi ya 50 wakitekwa katika shambulizi hilo linalodaiwa kutekelezwa na kundi la kijihadi la JNIM linaloshirikiana na Al-Qaeda.
Jeshi la Mali, limesema katika taarifa yake ya hivi punde kuwa, linaendelea na operesheni ya angani na ardhini kuwasaka washambuliaji waliolenga kambi hiyo ya Dioura.
Aidha, jeshi limesema, wavamizi hao waliwasili kwa pikipiki na kuanza kufwatua risasi ndani ya kambi hiyo, huku baadhi yao wakiuawa. Mwaka uliopita, shambulizi kama hili lilitokea katika kambi hiyo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.