Nchini Marekani, Mahakama ya Juu imekataa mpango wa rais Donald Trump, kupunguza kwa kiasi kikubwa upigaji kura kupitia njia ya posta, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Katikati wa Muhula mwezi Novemba.
Hili ni pigo kubwa kwa Trump, ambaye mwezi Machi aliangiza Shirika la Posta kuwasilisha karatasi za wapiga kura kwa Wamarekani waliothibitishwa kupiga kura.
Aidha, Trump alidai kuwa matumizi ya Posta kusafirisha kura, zilizopiwgwa, kunasababisha wizi wa kura.
Hata hivyo, Majaji walio wengi katika maamuzi ya kesi hiyo, wamesema kutekeleza agizo hilo la Trump, kutatiza zoezi la upigaji kura ambalo limeanza katika baadhi ya majimbo.
Kabla ya uamuzi huu, wasimamizi wa kura walikuwa wameonya kuwa, mabadiliko yoyote ya kuzuia wapiga kura kwa sasa kutumia njia ya Posta kupiga kura, kutasababisha zoezi hilo kutiliwa shaka na karatasi za wapiga kura kutowafikia wahusika kwa wakati.
Baada ya uamuzi wa Mahakama, wapiga kura nchini Marekani wataendelea kupokea karatasi zao kwa njia ya Posta na kupiga kura ya mapema kama miaka iliyopita.