Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, ameapa kuchukua kila sehemu ya ardhi ya nchi yake iliyo chini ya udhibiti wa wapiganaji wa RSF, huku akikataa majadiliano yanayolenga kumaliza vita iliyodumu kwa miaka mitatu na nusu.
Burhan alitoa kauli hii wakati alipokuwa akizungumza na raia kwenye kijiji kimoja kilichoko kaskazini mwa mji wa Merowe.
Kiongozi huyo amenukuliwa akisisitiza kuwa nguvu ya kijeshi itaendelea kutumiak hadi pale wapiganaji wa RSF watakapoondoka kwenye maeneo yote wanayoyakalia.
Kauli yake ameitoa wakati huu watu zaidi ya 10 wakiripotiwa kuuawa kwenye eneo la Kordofan Magharibi kufuatia mashambulizi ya RSF.
Mwezi uliopita wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema si jeshi la Sudan, wapiganaji wa RSF wala viongozi wao waliwasilisha mpango halali wa kuelekea kurejesha utawala wa kikatiba, kauli ya Burhan ikiwa pigo kwa juhudi za upatanishi.