Watu wanane wameuawa katika shambulio la Al Shabab

Watu wenye silaha wanaoshukiwa kutoka kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia, wamewauwa watu wanane, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Ripoti za polisi zimesema waliouwa ni pamoja na askari wawili wa akiba, dereva na wafanyakazi watano raia wa kawaida waliokuwa wanafanya kazi za ujenzi.

Watu hao walishambuliwa kwa kushtukiza katika Barabara ya kutoka Arabia kwenda Lafey, katika Kaunti ya Mandera inayopakana na nchi ya Somalia siku ya Jumanne.

Mashambulizi kama haya katika Kaunti ya Mandera, yamekuwa yakitekelezwa na magaidi wa Al-Shabaab.

Mwezi Julai, watu watano, wakiwemo maafisa wanne wa polisi waliuawa naada ya washukiwa wa Al Shabab kuwashambulia karibu na mji wa Lafey, umbali wa Kilomita 10 kutoka mpaka wa Kenya na Somalia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii