Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, limezuia mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) uliopangwa kufanyika ukumbi wa Milllenium Tower Kijitonyama jijini hapa.
Mkutano huo ulipangwa kuhutubiwa leo Juni 17,2025 na Makamu Mwenyekiti wa Chadema ( Bara), John Heche ambaye hadi saa 4:45 alikuwa hajafika hotelini hapo kwa ajili ya kuzungumza kwenye mkutano huo.
Wakati waandishi wakiwa tayari wamekusanyika wanamsubiri Heche katika ukumbi wa uliopo ghorofa ya tano, ndipo akaja Brenda Rupia ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi wa Chadema akabadilishana mawazo baadhi wanahabari kisha kuketi pembeni mwa meza kuu.
Ghafla wakaingia maofisa wa Polisi watatu mmoja akiwa amevaa sare waliojitambulisha wanatoka Kinondoni na Kanda Maalumu Dar es Salaam, wakauliza nani muhusika wa mkutano huo.