Watoto Tisa Wazaliwa Mkesha wa Krismasi Tarime

Watoto tisa wavulana watano na wasichana wanne wamezaliwa salama usiku wa mkesha wa Krismasi katika Hospitali ya Halmashauri ya Tarime Mjini mkoani Mara.

Kwa mujibu wa Umoja wa Waandishi wa Habari Wilaya ya Tarime (REU) uliwakabidhi wazazi zawadi kama ishara ya faraja na kushiriki furaha ya Krismasi.

Muuguzi Mwandamizi Mary Wilson alisema watoto hao walizaliwa kwa njia ya kawaida na aliishukuru REU kwa kuwasaidia wagonjwa waliolazwa katika wodi mbalimbali za hospitali.

Aliwataka wazazi kuendelea na kliniki ili watoto wapate chanjo na vyeti vya kuzaliwa.

Mzazi Maryamu Rashidi aliishukuru serikali na REU kwa mazingira mazuri ya huduma baada ya kujifungua mtoto wa kiume Desemba 24 mwaka huu.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii