Mkazi wa Kimara aeleza jinsi Vicoba ‘ilivyouza’ nyumba yake kimakosa

MKAZI wa Kimara Sara Mtoka ameeleza namna kikundi cha kukopeshana fedha cha wanawake (VICOBA) kilivyosababisha nyumba yake kuuzwa kimakosa.

Mtoka alieleza hayo jana Mbagala alipofika kwenye Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwa ajili ya kupata msaada wa kurejeshewa nyumba yake.

Alidai mwaka 2012 alikuwa amejiunga na kikundi cha akinamama ambacho walikuwa wakishirikiana na kusaidiana, kukopesha na kukuza biashara zao.

Allifafanua kuwa siku moja, mmoja wao aliwafahamisha kwamba anahitaji kudhaminiwa kwa ajili ya mkopo. Kwa kuwa walikuwa wanaaminiana, walimdhamini.

Alisimulia kuwa nyumba yake iliwekwa mnada akiwa safarini na binti yake ndiye aliyeitwa na kushinikizwa kutia saini.

Alisema kuwa baada ya kurejea, alifungua kesi katika Mahakama ya Ardhi na kushinda lakimi mnunuzi wa nyumba aliendelea kudai kuwa yeye ni mmiliki halali na akawasilisha hati ya makazi ili asiondolewe kwenye nyumba.

Aidha alisema kuwa hakuwa na mwanasheria bali alibahatika kupata wakili aliyemsaidia kupeleka kesi yake Mahakama Kuu ambapo mwaka 2022 alishinda lakini ili hukumu itekelezwe, ilibidi awalipe madalali wa mahakama Sh milioni sita ili waondoe wapangaji waliopo kwenye nyumba hiyo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii