MSD yataja hatua za uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa za ndani

Bohari ya Dawa (MSD) imesema uwekezaji katika uzalishaji wa bidhaa za afya ndani ya nchi unahitaji kuimarishwa ili viwanda vizalishe zaidi, kukidhi mahitaji ya nchi na kuliingizia Taifa fedha za kigeni.

Imesema utegemezi wa uagizaji wa bidhaa za afya, unatokana na uwezo hafifu wa viwanda vya ndani, uwekezaji katika sekta ya viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo, hali inayosababisha zaidi ya asilimia 80 huagizwa kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai wakati wa Kongamano la Kitaifa la Tiba na Maadhimisho ya miaka 60 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) linalofanyika leo Ijumaa Juni 20, 2025 jiini hapa.

Amesema ili kupambana na changamoto hiyo, MSD imeanza michakato mbalimbali ya kuhakikisha dawa muhimu zinazalishwa ndani ya nchi kupitia viwanda vilivyopo, kwa kuvielekeza bidhaa zipi viongeze kulingana na uwezo wa uzalishaji na hivyo wamekuwa wakifanikiwa kupunguza utegemezi wa nje.

Tukai amesema nchi za Jangwa la Sahara zina uhitaji mkubwa wa bidhaa za afya, lakini ili kufikia matarajio walifanya tafiti kadhaa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii