Rais Samia asisitiza umuhimu na jitihada za kuhifadhi mazingira Ziwa Victoria

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza jitihada za kuhifadhi mazingira ziendelee kufanyika kikamilifu kwa kushirikiana na sekta zote nchini na kwamba ni muhimu kulinda mazingira hasa Ziwa Viktoria ili liendelee kuwepo kwa hali bora na lisikauke.

Ametoa agizo hilo Juni 20, 2025 muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa maji wa Butimba jijini Mwanza, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.

Rais Samia amesema kuwa  mradi huu ni mkubwa hivyo lazima kutunza mazingira ili ziwa hili liendelee kuwepo kwa vigezo vyake pasipo kukauka ili kuepuka  kutotukarudi nyuma kimiundombinu kwani uwekezaji  uliofanywa ni wa gharama kubwa sana, hivyo wote washirikiane kulinda mazingira.

Aidha amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu nchini ili kuwezesha maendeleo kuendelea kwa mafanikio, huku akisisitiza kuwa utashi wa kisiasa wa kuleta maendeleo upo na utaendelea kuwepo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii