Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Benedicto Ngaiza, amewataka wataalamu wa sekta ya afya ea mikoani ya Mtwara, Lindi na Wilaya ya Tunduru kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kulipa Madeni ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuipa msuli wa kiuchumi katika kutekeleza majukumu yake katika mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa weledi ufanisi na kwa wakati.
Dkt. Ngaiza amesema kutolipa madeni ya MSD kwa wakati kunadhoofisha juhudi zinazofanywa na MSD na serikali kwa ujumla kuboresha huduma za afya nchini mathalani upatikanaji wa bidhaa za afya.
Dkt.Ngaiza ametoa rai hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa ufunguzi wa kikao cha wateja na wadau wa MSD Kanda ya Mtwara kwa mwaka 2025 kilichofanyika Mkoani Mtwara.