Baraza la Madiwani kuvunjwa rasmi juni 20 mwaka huu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa ametangaza kuwa mabaraza yote ya madiwani nchini yatavunjwa rasmi ifikapo Juni 20, 2025.

Tangazo hilo amelitoa  Juni 15, 2025 alipokuwa akitoa tamko rasmi kuhusu tarehe ya kuvunjwa kwa mabaraza hayo pamoja na mikutano ya kamati za kudumu za halmashauri.

Kwa mujibu wa Mchengerwa mamlaka hayo yametolewa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa na Mamlaka za Wilaya Sura ya 287 kifungu cha 178 ambacho kinamruhusu Waziri mwenye dhamana kuvunja mabaraza hayo siku saba kabla ya Bunge kuvunjwa kuelekea uchaguzi mkuu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii